Rais William Ruto wa Kenya na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni,siku ya Jumamosi wamezindua awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Kisumu hadi Malaba.
Reli hiyo ya umbali wa kilomita 107, itaunganishwa na ile ya kutoka Mombasa ikijumuisha umbali wa kilomita 1,000, kutoka Mombasa hadi Malaba na kuingia nchini Uganda.
Rais Ruto alisema reli hiyo itapanua fursa za kibiashara na kurahisisha usafiri kati ya Kenya na Uganda.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya Rais pia kuzindua ujenzi wa kilomita 264, za reli ya SGR kutoka Narok hadi Kisumu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wakuu kutoka serikali zote mbili.