Ruto kuelekea Ujerumani Jumapili usiku

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto

Rais William Ruto anatarajiwa kuondoka nchini Jumapili usiku kuelekea nchini Ujerumani kwa ziara rasmi ya serikali.

Ziara ya Rais Ruto nchini Ujerumani itakuwa ya 41 kwa jumla tangu atwae madaraka mwaka uliopita.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili iliyoandaliwa katika kanisa moja katika kaunti ya Bomet, Ruto alitetea ziara zake ugaibuni akisema lengo lake ni kutafuta ushirikiano wa kimataifa utakaowanufaisha Wakenya.

Aidha Naibu wake Rigathi Gachagua ametetea vikali ziara hizo na kuahidi kuandaa ripoti ya manufaa yake kwa nchi hivi karibuni.

Kunao ambao wameshutumu ziara za Rais Ruto nje ya nchi mara kwa mara wakizitaja kuwa matumizi mabaya ya rasilimali za umma hasa wakati nchi inakabiliwa na changamoto za kiuchumi.

Wakenya wanalalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na hasa kupanda kwa bei ya mafuta mwezi baada ya mwezi kumekuwa kero kwa wengi.

Website |  + posts
Share This Article