Rais Ruto ainadi Kenya kwa wawekezaji wa Marekani

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto amesema serikali ya Kenya inaboresha sheria na sera za taifa hili ili kukidhi mahitaji ya wawekezaji wa kimataifa. 
Ruto amesema mazingira yaliyoboreshwa ya kibiashara pamoja na nguvu kazi iliyoelimika na kupata mafunzo bora sambamba na rasilimali nyingi za nishati mbadala zinaifanya Kenya kuwa mahali bora pa kufanya biashara na uwekezaji.
“Kwa kusikiliza kwa makini sekta ya binafsi, tunahakikisha sera zetu zinasalia kuwa zinazostahiki na bora,” alisema Ruto.
Aliyasema hayo wakati wa kongamano la kibiashara na uwekezaji kati ya Kenya na Marekani lililoandaliwa na Baraza la Mashirika juu ya Afrika pembezoni mwa kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Newa York nchini Marekani.
Rais Ruto alitoa wito kwa wawekezaji nchini Marekani kuchukua fursa ya mazingira bora ya biashara na kuwekeza humu nchini.
“Nawakaribisha nchini Kenya na kuwahakikishia kuwa nitawezesha kuingia kwenu kwenye soko la nchi hiyo bila matatizo,” aliongeza Ruto.
Share This Article