Mwanamuziki wa Tanzania Raymond Shaban maarufu kama Rayvanny amezungumzia suala la kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye pia ni mama ya mtoto wake Fahyma.
Baada ya kutangaza awali mitandaoni kwamba mwaka huu anaoa na atamwoa Fahyma, Vanny Boy sasa amesema kwamba Fahyma hajawahi kumwomba ndoa.
Kulingana naye, Fahyma ndiye amekuwa akiahirisha ndoa yao kwa kudai kwamba yeye bado ni mdogo, huku akimsifia kwamba yeye ni mvumilivu na ana heshima.
“Mungu akijalia niliyoyasema yatatimia.” alisema Rayvanny akirejelea machapisho yake ya wiki chache zilizopita kuhusu Fahyma ambapo alikiri mapenzi yake kwake na kuahidi kumwoa.
Rayvanny alichapisha picha ya Fahyma na kuandika, “Kama nilikuchezea samahani, huyu ndiye mke wangu nampenda kuliko chochote kile, yeye ni kila kitu kwangu nampenda sana Fahyma maisha yangu. TAMKO RASMI NAOA MWEZI WA 5”.
Msanii huyo alikuwa anajibu maswali kutoka kwa wanahabari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam nchini Tanzania punde baada ya kuongoza tukio la kampuni ya kamari ya Piga Bet.