Kinara wa shirikisho la soka nchini (FKF),Hussein Mohamed, ameitisha kikao na Wanahabari siku ya Jumatatu, ili kufafanua kuhusu hatima ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Sportpesa.
Msimu wa mwaka 2026/2026 uliokuwa uanze mapema mwezi huu tayari umecheleweshwa kwa majuma matatu.
Korti iliamua kuanza kwa ligi hiyo Jumamosi iliyopita lakini wasimamizi wa Ligi wakasitisha dakika za mwisho wakitaja kuwa kulikuwa na baadhi ya masuala ambayo hawakuwa wameafikiana.
Utata wa ligi hiyo unatokana na kesi kadhaa ambazo zimewasilishwa mahakamani kutoka kwa klabu ambazo hazikuridhishwa na mfumo wa kupandishwa na kushushwa ngazi ligini.