Waziri wa kawi Opiyo Wandayi ametetea mpango wa serikali ya Kenya wa kuagiza mafuta wa G to G, huku akikanusha madai yaliyoibuliwa na serikali ya Uganda.
Wandayi amesema mpango huo ulianzishwa kama njia ya kukabiliana na ongezeko la bei ya Dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya humu nchini na pia upungufu wa dola katika soka.
Waziri ameongeza kuwa kutokana na mpango huo bei ya bidhaa za mafuta humu nchini zimedhibitiwa,akisisitiza kuwa bei hiyo ingepanda zaidi bila mbinu hizo mwafaka za serikali.
Aliongeza kuwa mpango wa G to G umeisaidia serikali kuwa na akiba tosha ya dola na kudhibiti bei ya shilingi dhidi ya dola.
Matamshi ya Wandayi yanajiri wakati serikali ya Uganda imebua hofu yake kuhusiana na mpango wa G to G.