Rais Trump awasili China kwa ziara ya kiserikali

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais wa Marekani Donald Trump, amewasili Jijini Beijing Jumatano jioni kwa ziara ya kiserikali nchini China.

Hii ni ziara yake ya kwanza nchini China katika muda wa miaka tisa, na ya pili tangu mwaka 2017.

Ndege ya Air Force One ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Beijing, muda mfupi kabla ya saa mbili usiku, ambapo Trump alilakiwa na makamu Rais wa China Han Zheng na kuandaliwa gwaride ya kijeshi, tamasha na kukaribishwa na watoto waliopeperusha bendera.

Kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping,  ziara ya Trump itaanza Mei 13 hadi 15, huku ikiangazia uhusiano wa nchi hizo mbili, amani duniani na maendeleo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana Alhamisi na Ijumaa, mazungumzo yao yakilenga uhusiano wa kibiashara kati ya chumi hizo mbili kubwa duniani na mzozo unaoghubika Iran.

Share This Article