Tuwei amwomboleza Malboum

Marehemu ameongoza shirikisho la Riadha Afrika tangu mwaka 2003, na alikuwa akamilishe muhula wa sita mwaka ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read
Marehemu Hamad Kalkaba Malboum

Rais wa chama cha Riadha nchini Kenya, Jackson Tuwei, amemwomboleza Rais wa shirikisho la Riadha Afrika, Hamad Kalkaba Malboum, kutoka Cameroon, aliyeaga dunia mapema Jumatano.

Tuwei alimtaja marehemu kuwa kiongiozi aliyejitolea na aliyeleta maendeleo mengi katika riadha kote barani Afrika.

Tuwei ambaye alikuwa Naibu wa Kalkaba alisoma risala za rambirambi akiandamana na Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani, Sebastien Coe, jijini Accra,Ghana, Jumatano jioni katika mashindano ya Afrika yanayoendelea .

Kando na kuwa naibu ,Kalkaba, alikuwa kwenye baraza la shirikisho la Riadha Duniani, wakihudumu pamoja na Tuwei.

Kalkaba alifariki dunia Jumatano akiwa na umri wa miaka 75,baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Marehemu ameongoza shirikisho la Riadha Afrika tangu mwaka 2003, na alikuwa akamilishe muhula wa sita mwaka ujao.

Share This Article