Wakenya Dorcas Ndiema na Mercy Chepkemoi, walenga nishani Accra leo

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 mjini Doula,Cameroon ilikomaliza ya pili nyuma ya Afrika Kusini kwa nishani 19,dhahabu 5 fedha 7 na shaba 7.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya inatarajia kuzoa medali katika siku ya kwanza ya makala ya 24, ya mashindano ya Riadha Barani Afrika, yaliyoanza leo mjini Accra,Ghana.

Mercy Chepkemoi na Dorcas Ndiema, wataipeperusha bendera ya Kenya, katika fainali ya mita 5,000, itakayoanza saa tatu kasoro dakika kumi usiku.

Chepkemoi na Ndiema, waliomaliza katika nafasi za pili na tatu kwenye mashindano ya Kip Keino Classic mwezi uliopita, watalenga kurejesha taji hiyo ambayo Kenya ilipoteza mwaka 2024.

Mashindano mengine yatakayowashirikisha Wakenya usiku huu ni raundi ya kwanza ya mita 800 wanaume ambapo kelvin Kimtai,Brian Musyoka na Laban Chepkwony, watawania tiketi ya nusu fainali.

Wakenya pia wanashiriki michujo ya mita 100 wanaume na mita 400 kwa wanaume na wanawake

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 mjini Doula,Cameroon, ilikomaliza ya pili nyuma ya Afrika Kusini kwa nishani 19,dhahabu 5 fedha 7 na shaba 7.

Share This Article