Rais Trump ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Martin Mwanje
1 Min Read
Donald Trump - Rais wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa miongoni mwa viongozi wa dunia waliohutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani jana Jumanne. 

Kwenye hotuba yake, Trump alizungumzia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita nchini Iran na Ukraine.

Huku akielezea hadhira kwamba ana uamuzi mkubwa wa kufanya kuhusu vita hivyo, Trump alisema anatarajia Marekani na Iran kufikia makubaliano baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula utakaofanywa mwezi Novemba.

Vita kati ya Marekani na Iran vilianza Februari 26 mwaka huu baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Trump pia alizungumzia uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine akiashiria anafanya kazi kwa karibu na viongozi wa nchi hizo mbili kusuluhisha mzozo huo.

Aliahidi kuwa utawala wake utahitimisha mzozo huo haraka mno.

Kadhalika, kiongozi huyo wa Marekani alizungumzia teknolojia ya akili unde, AI akisema nchi yake inakataa katakata jitihada zozote za kuidhibiti teknolojia hiyo.

Aliongeza kuwa Marekani iko mbele ya China na mataifa mengine katika AI na kwamba nchi yake itaongoza dunia kwa usalama na uwajibikaji katika kile alichokiita ‘akili ya kiwango cha juu zaidi.’

 

Share This Article