Rais suluhu akutana na Katibu Mkuu wa EAC Veronica Nduva

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu leo Jumatatu amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronica Nduva.

Wawili hao walikutana wakati Nduva alipomtembelea Rais Suluhu katika Ikulu ya nchi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Wawili hao wameripotiwa kuzungumzia mbinu zinazoweza kutumiwa kuboresha utendakazi wa jumuiya hiyo kwa manufaa ya raia wa Afrika Mashariki miongoni mwa mambo mengine.

Hii ni mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana tangu Nduva aliposhika wadhifa huo mwezi Juni mwaka huu.

Nduva aliteuliwa Katibu Mkuu wa EAC ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake Dkt. Peter Mathuki.

Share This Article