Rais Suluhu afanya ziara nchini Uganda

Suluhu anafanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais Samia Suluhu akiwasili nchini Uganda

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amewasili katika nchi jirani ya Uganda kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili. 

Suluhu anafanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

“Nchi zetu zina uhusiano wa kidugu na kihistoria uliojengwa kwa miaka mingi,” amesema Rais Suluhu wakati akianza ziara hiyo.

“Ziara hii inalenga kuimarisha zaidi uhusiano huo na kufungua fursa mpya za ushirikiano, zitakazonufaisha wananchi wa nchi zetu kiuchumi na kuchagiza maendeleo ya mataifa yetu.”

Share This Article