Jaji wa ICC kutoka Uganda Solomy Bossa, awekewa vikwazo vya usafiri na Marekani

Bossa ni miongoni mwa Majaji wanne wa ICC waliowekewa vikwazo hivyo na Marekani .

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Rais Donald Trump ya Marekani, imemwekea vikwazo vya usafiri Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ICC, Solomy Balungi Bossa kutoka Uganda.

Hii inafuatia hatua ya Mahakama ya ICC kutoa amri ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Vikwazo hivyo vinajumuisha kuzuiwa kusafiri kuingia Marekani, kuzuia kutoa fedha au kufanya muamala katika benki yoyote aliyoihifadhi pesa inayomilikiwa na Mrekani.

Bossa ni miongoni mwa Majaji wanne wa ICC waliowekewa vikwazo hivyo na Marekani .

Website |  + posts
Share This Article