Rais Suluhu afanya mabadiliko ya Mawaziri

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amelifanyia mabadiliko Baraza lake la Mawaziri.

Kwenye mabadiliko hayo, Profesa Palamagamba Kabudi aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akitokea Wizara ya Katiba na Sheria.

Innocent Bashungwa aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya Hamadi Masauni. Awali, Bashungwa alikuwa akihudumu kama Waziri wa Ujenzi.

Rais Suluhu pia alimhamisha Dkt. Damas Ndumbaro kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hadi ile ya Katiba na Sheria akibadilishana Wizara na Prof. Kabudi.

Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi huku aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Abdallah Ulega akipelekwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Jerry Silaa ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akiondolewa jukumu la sekta ya habari ambalo sasa limerudi kwenye Wizara ya Michezo kama ilivyokuwa awali.

Rais Suluhu pia alifanya mabadiliko ya Makakatibu wa Wizara huku walioteuliwa wakila kiapo katika ikulu ndogo kisiwani Zanzibar.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *