Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki mazungumzo na mfanyabiashara kutoka nchini Nigeria Alhaji Aliko Dangote pamoja na Ujumbe wake, katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Dangote, ni Mwanzilishi na Mmiliki wa kampuni ya Dangote Group.
Mkutano wa wawili hao ni wa pili mwaka huu, huku wakikutana awali Machi 16, 2026, majadiliano yao wakati huo yakilenga uwekezaji na ujenzi wa kiwanda cha mafuta.
Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumapili na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bakari Machumu, mfanyabiashara huyo alielezea lengo la kampuni yake kupanua ushirikiano na serikali ya Tanzania katika sekta nishati, uzalishaji na usafirishaji wa mbolea.
Kwenye taarifa hiyo, Dangote alidokeza kuwa Tanzania inadizi kuwa na mazingira bora ya uwekezaji Afrika, kutokana na fursa zilizopo katika sekta za uzalishaji na viwanda.
Kwa upande wake, Rais Samia alikaribisha mapendekezo ya Dangote, huku akitoa wito kwa taasisi husika za serikali kufanikisha yaliyojadiliwa kwa kuzingatia sera zilizopo na kuambatana na sheria.
Rais Samia alisema serikali yake itashirikiana kwa karibu na sekt ya kibinafsi, kubuni nafasi za ajira kwa raia wa taifa hilo.