Wafanyabiashara wa usafirishaji wa makontena kutoka bandari ya Mombasa wangali wanakadiria hasara huku mgomo wa madereva wa malori ukiingia siku ya tatu.
Madereva wanapiga agizo la serikali kupitia kwa mamlaka ya usalama barabarani, NTSA kutekeleza sharti la kila dereva kutathminiwa upya kila wakati wa kutafuta leseni mpya.
Makontena pekee yaliyosafirishwa ni yale ya kupitia reli ya SGR ambayo inamudu makontena 1,500 pekee wakati malori yakisafirisha makontena 4,000 kwa siku.
Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen Jumanne wiki hii alitoa agizo la kufutilia mbali mgomo huo, agizo ambalo limepuuzwa na madereva hao.