Rais Ruto: Serikali itahakikisha SHA ina pesa za kutosha kuwahudumia wakenya wote

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto amedumisha kwamba hazina mpya ya bima ya kijamii-SHIF inatarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakenya wote.

Akiongea wakati wa tamasha la kitamaduni la jamii ya wamaasai katika hifadhi ya kitaifa ya Samburu, rais Ruto alisema serikali imejitolea kuzingatia katiba kwa kuhakikisha kwamba familia kutoka jamii zisizojiweza zina fursa sawa ya kupata huduma za matibabu.

Alisema serikali itahakikisha kwamba halmashauri ya SHA ina pesa za kutosha kuwahudumia wakenya wote, akiongeza kwamba kuanzia sasa kuendelea, hakuna hakuna atakayelazimika kulipa pesa ili kupokea matibabu katika hospitali za umma.

Aidha kiongozi wa taifa aliwahakikishia wakenya kwamba serikali tayari imesuluhisha changamoto zilizokuwa wakati wa kuzindua mfumo wa SHIF.

Wakati uo huo, Rais alihimiza jamii zinazoishi katika kaunti ya Samburu kusitisha wizi wa mifugo.

Rais Ruto alisema serikali ya kitaifa inajitahidi kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo la wizi wa mifugo katika kaunti ya Samburu.

Share This Article