Rais Ruto awatakia kila la heri watahiniwa wa KCPE na KPSEA

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto katika shule ya msingi ya Kikuyu Township, kaunti ya Kiambu.

Rais William Ruto Jumatatu asubuhi aliongoza zoezi la ufunguzi wa karatasi za mitihani ya kitaifa ya darasa la nane  KCPE na ile ya tathmini ya gredi ya sita KPSEA, katika shule ya msingi ya Kikuyu Township kaunti ya Kiambu.

Rais aliwatakia watahiniwa wote hapa nchini kila heri wanapofanya mitihani, akisema serikali imeweka mikakati kuhakikisha wanajiunga na kidato cha kwanza na gredi ya saba bila matatizo.

“Nawatakia kila la heri, baraka za Mwenyezi Mungu na ushindi mkubwa,”alisema Rais Ruto.

Rais aliwahakikishia watahiniwa kwamba uongozi wa taifa upo pamoja nao huku akiwapongeza walimu kwa jukumu muhimu wanalotekeleza la kuwaandaa wanafunzi.

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka huu unakunja jamvi la mtaala wa elimu wa 8-4-4, huku mtaala mpya wa CBC ukichukua usukani.

Share This Article