Rais William Ruto amewasili katika Uwanja wa Kwale kunakoandaliwa sherehe za mwaka huu za Siku ya Mashujaa.
Rais alilakiwa na Naibu Rais mteule Prof. Kithure Kindiki na Gavana wa kaunti hiyo Fatuma Achani punde baada ya kuwasili katika uwanja huo.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Magavana kutoka eneo Pwani, Mawaziri, Makatibu na Mabalozi tayari wamewasili katika uwanja huo.
Kaulimbiu ya sherehe hizo ni “Boma Langu, Nyumba Yangu, Mimi ni Shujaa.”