Rais Ruto awasili Qatar kwa mkutano wa UN kuhusu Maendeleo ya Jamii

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William awasili Jijini Doha Qatar.

Rais William Ruto amewasili jijini Doha, Qatar, kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu ustawi wa jamii.

Nchini Qatar, Rais Ruto atahudhuria Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa, UN Juu ya Ustawi wa Jamii (WSSD2) ambao utaangazia uangamizaji umaskini, kazi nzuri na ujumuishaji katika jamii.

“Akiwa nchini Qatar, Rais Ruto will atahitimisha makubaliano ya uwekezaji muhimu ili kuifanya miundombinu ya Kenya kuwa ya kisasa na kuendeleza miradi muhimu ya nishati na uchukuzi,” ilisema taarifa iliyotumwa na msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed.

“Atafanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa dunia akiwemo His Highness Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Sheikh wa Qatar, ili kuimarisha ushirikliano katika biashara, uwekezaji, na mipango ya maendeleo ya kimkakati.”

Rais Ruto akilenga kutumia ziara hiyo kuendeleza uwekezaji uliopanuliwa na ushirikiano wa kimkakati na Qatar katika kilimo, hasa usalama wa chakula, nishati mbadala, afya, utalii na uchuk

Website |  + posts
Share This Article