EACC yazindua kampeni ya uhamasishaji dhidi ya ufisadi Kwale

Tom Mathinji
1 Min Read
EACC yazindua kampeni dhidi ya ufisadi kaunti ya Kwale.

Tume ya Maadili na vita dhidi ya Ufisadi (EACC), imezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi dhidi ya ufisadi katika kaunti ya Kwale.

Kulingana na EACC, lengo kuu la uhamasisho huo ni kukuza maadili na uwajibikaji miongoni mwa wananchi, hii ikiwa ni mojawepo wa majukumu ya tume hiyo ya kutoa mafunzo, kuwezesha na kuhamasisha wananchi dhidi ya ufisadi kuhakikisha kila mkenya anatekeleza jukumu la kufanikisha jamii yenye uwazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, katibu wa kaunti ya Kwale Sylvia Chidodo, alitoa wito kwa wakazi wa kaunti hiyo kukumbatia maadili, akidokeza kuwa taifa hili litapiga hatua kubwa iwapo maadili na uwajibikaji zitazingatiwa kikamilifu.

Naibu Mkurugenzi wa EACC anayehusika na elimu na uhamasishaji wa umma Dkt. Emily Mworia, alipongeza kaunti ya  Kwale kwa ushirikiano huo, akielezea kujitolea kwa EACC kushirikiana na kaunti zote kuimarisha uongozi bora.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article