Rais Ruto atoa hatimiliki 26,000 kwa wakazi wa Lunga Lunga

Hafla hiyo itaendelea hadi Jumamosi hii huku wakazi 300,000 wakitarajiwa kunufaika katika awamu hiyo ya kwanza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto mapema leo Jumatatu ameongoza hafla ya kutoa hatimiliki 26,000 kwa wakazi wa mtaa wa Kibaoni, eneo la Lunga Lunga, kaunti ya Kwale.

Akizungumza katika mtaa wa Kibaoni, Ruto alisema analenga kutoa hatimiliki nusu milioni kwa wakazi wa Pwani kama njia ya kumaliza tatizo sugu la uskwota.

Hafla hiyo itaendelea hadi Jumamosi hii huku wakazi 300,000 wakitarajiwa kunufaika katika awamu hiyo ya kwanza.

Kaunti ya Taita Taveta imetengewa hatimiliki  31,318, Kwale  hatimiliki 94,175, Kilifi hatimiliki 36,826, huku Mombasa ikitengewa hatimiliki 4,360 wakati Lamu na Tana River zikitarajiwa kupokea jumla ya hatimiliki 22,770.

Viongozi wa eneo la Lamu ikiwa ni pamoja na Gavana Fatuma Achani na Waziri wa Michezo Salim Mvurya wamehudhuria hafla hiyo.

Share This Article