Rais Ruto ashauriana na viongozi kutoka Nyanza

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto na viongozi wa Nyanza katika Ikulu ya Nairobi.

Rais William Ruto, amesema utawala wake utafanya kazi na viongozi kutoka pembe zote za nchi, bila kuzingatia miengemeo yao ya kisiasa ili kuwahudumia wakenya.

Akizungumza Jumanne katika Ikulu ya Nairobi alipokutana na wabunge kutoka eneo la Nyanza, kiongozi wa taifa alisema serikali ya Kenya Kwanza, itakumbukwa kwa miaka mingi kwa kuwahudumia wakenya kwa njia ya haki na usawa.

“Tutafanya kazi na viongozi kote nchini bila ubaguzi na bila kuzingatia miegemeo yao ya kisiasa, ili kuwahudumia wakenya. Hii ni kwa mujibu wa Katiba na ni haki ya wakenya,”alisema Rais Ruto.

Viongozi hao walijadili kuhusu mipango na miradi ya serikali yanayoendelea kwa sasa katika eneo la Nyanza.

Viongozi hao walijumuisha Gideon Ochanda Mbunge wa Bondo, Seneta wa Kisumu Tom Ojienda, mbunge wa Suba Mashariki  Caroli Omondi,  Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo na mbunge wa Uriri Mark Nyamita.

Wengine ni pamoja na mbunge wa Rongo Paul Abuor, na mbunge wa Langáta  Felix Odiwuor.

Waziri wa habari na mawasiliano Eliud Owalo na katibu katika wizara ya usalama wa taifa Raymond Omollo, pia walihudhuria.

Website |  + posts
Share This Article