Rais Ruto ashauriana na Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amesema ameshauriana na rais mteule wa Marekani Donald Trump kwa njia ya simu kuhusiana na shughuli ya kudumisha amani nchini  Haiti inayoongozwa na polisi wa Kenya.

Kwenye taarifa kupitia mtandao wa X, kiongozi wa taifa alisema wakati wa mazungumzo hayo alimuarifu pia Rais Trump kuhusu uwezekano wa ushirikiano katika sekta mbalimbali na serikali ya Marekani kuhusu mpango muhimu wa kutatua mzozo nchini humo.

“Nilimpongeza kufuatia ushindi wake wa kuwa Rais wa 47 wa Marekani. Tulijadiliana kuhusu maswala mengine yanayowahusu raia wa nchi hizo mbili,”alisema Rais Ruto.

Hayo yanajiri huku Inspekta Jenerali wa polisi, Douglas Kanja akithibitisha kuwa kikosi kipya cha maafisa 600 wa polisi, kiko tayari kupelekwa nchini Haiti ambapo kinadhamiria kurejesha amani na kudumisha uthabiti nchini humo.

Akiongea Ijumaa alipofunga rasmi mafunzo ya maafisa wa usalama watakaolekea Haiti kudumisha amani katika chuo cha kitaifa cha polisi,bewa la  Embakasi ‘A’ ,Kanja alisema maafisa hao wa polisi wanatoka kutoka kitengo cha GSU,kile cha kupambana na uhalifu pamoja na kile cha  RDU,wale wa silaha maalum na kikosi cha kiufundi.

Kanja alisema taifa hili tayari limepeleka kikundi cha kwanza cha polisi cha takriban maafisa-400 nchini   Haiti.

Website |  + posts
Share This Article