Rais William Ruto, amesaini kuwa sheria muswada wa fedha wa mwaka 2025,kwenye hafla iliyoandaliwa mapema leo katika Ikulu ya Nairobi.
Sheria hiyo italeta mabadiliko kadhaa mapya ingawa hakuna ushuru mpya ulioongezwa kwa bidhaa za kawaida za matumizi.
Wasindikaji na wakulima wanatarajiwa kunufaika kutoka na kuondolewa kwa ushuru wa bidhaa ghafi,na vifaa vya kupakia chai na kahawa.
Aidha,sheria hiyo pia itashuhudia kujumuishwa kwa ushuru mpya kwa kamari na huduma za kidijitali.