Rais Ruto ampongeza Faith Kipyegon

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto amempongeza mwanariadha shupavu Faith Kipyegon kufuatia ushindi wake kwenye mbio za mita 1500 za mashindano ya Diamond League huko Paris Ufaransa.

Kiongozi wa nchi amemsifia Kipyegon ambaye pia alivunja rekodi ya dunia ya mbio hizo kupitia ushindi wake akisema kwamba ameandikisha historia kwa mara nyingine.

“Pongezi kwa kuvunja rekodi yako mwenyewe katika mbio za mita 1500. Ushindi wako ni ushuhuda wa mazuri yanayotokana na bidii na kujitolea.” aliandika Rais kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Aliongeza kwamba ushindi wa Kipyegon ni funzo kuu kwa wanariadha chipukizi ambao wanamtizama kama mfano wa kuigwa.

Rais Ruto aliwapongeza pia wanariadha wa Kenya Amos Serem na Abraham Kibiwott ambao walinyakua nafasi za pili na tatu mtawalia katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji.

“Tunajivunia timu ya Kenya kwa uwakilishi mwema katika mashindano ya Paris ya Diamond League.” alimalizia kiongozi wa nchi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *