Rais Museveni apokea mwafaka wa Butiama kutoka kwa Mashariki Fest

Dismas Otuke
2 Min Read
Dkt.Ronex Kisembo (kushoto) akiwasilisha nakala ya mwafaka wa Butiama kwa Rais Museveni

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika la Afrika Mashariki Fest Dkt. Kisembo Ronex Tendo alikutana na Rais Yoweri Kaguta Museveni jana katika ikulu ya Entebe na kumkabidhi nakala ya mwafaka wa   Butiama accord, maarufu kama azimio la Butiama.

The Butiama lilisainiwa katika makao ya hayati marehemu Rais mwanzilishi wa Tanzania Julius Nyerere mtaani Butiama tarehe 14 mwezi huu.

Mwafaka wa Butiama ambao utawasilishwa kwa kongamano la Marais wa Afrika Mashariki mjini Arusha Tanzania ,Disemba mwaka huu linajumuisha maoni ya zaidi ya vijana milioni  laki mbili kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki waitakayo na jinsi ya kuafikia utangamano wa jumuiya.

Dkt .Kisembo aliandamana na Neema Nyerere mwakilishi wa familia ya Mwalimu Nyerere, na vijana waakilishi kutoka mataifa yote manane wanachama wa EAC walishuhudia hafla hiyo ya kukabidhi mwafaka wa Butiama kwa Rais Museveni.

Dkt. Kisembo pia aliwasilisha kitabu cha ukumbusho wa 25 wa marehemehu Nyerere kilichosainiwa na Marais wote wanane wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwafaka huo unataka kuondolewa kwa vizingiti wa utangamano wa jumuiya ikiwemo kuondolewa kwa visa za usafiri ndani ya jumuia

Matakwa mengine katika mwafaka huo ni kuwa na: Ndege moja ya usafiri,kuwa na halmashauri moja ya kutangaza utalii wa jumuia na kuwa na sarafu moja kwa mataifa manane ya Afrika Mashariki.

Licha ya kubuniwa miaka 25 iliyopita vikwazo baina ya mataifa wanachama vimezuia utangamano wa jumuiya , hali inayotishia muungano wa EAC.

Share This Article