Rais mpya wa Botswana Duma Gideon Boko ametangaza kundi la kwanza la Mawaziri sita siku chache baada ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Taarifa kutoka ofisi yake imeashiria kuwa Mawaziri wengine watatangazwa baadaye wiki hii.
Katika uteuzi huo, Ndaba Gaolatlhe ametangazwa kuwa Makamu wa Rais na Waziri wa Fedha huku Lesego Chombo akitangazwa kuwa Waziri wa Vijana na Masuala ya Jinsia.

Wizara ya Ustawi wa Watoto na Elimu ya Msingi itasimamiwa na Nono Kgafela-Mokoka wakati ile ya Mambo ya Nje ikidhibitiwa na Dkt. Phenyo Butale.

Dkt. Stephen Modise ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya huku Lawrence Ookeditse akiteuliwa kuwa Waziri Msaidizi.
Wizara ya Ardhi na Kilimo itasimamiwa na Dkt. Micus Chimbombi huku Dkt. Edwin Dikoloti akiteuliwa Waziri Msaidizi.