Rais Biden atetea uamuzi wake wa kutuma mabomu hatari Ukraine

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Joe Biden. Picha/Hisani.

Rais Joe Biden wa marekani ametetea uamuzi wake tata wa kuipa Ukraine mabomu yanayorushwa kwa pamoja ambayo husababisha vifo vya raia wengi.

Rais Biden alisema kuwa imemchukua muda kushawishiwa kuchukua hatua hiyo lakini alifanya hivyo kwa sababu Ukraine imeishiwa na risasi.

Hata hivyo waziri mkuu wa uingereza Rishi Sunak alipendekeza kwamba nchi hiyo isiruhusu utumiaji wa mabomu ya aina hiyo huku uhispania ikikosoa uamuzi huo.

Sunak alisema kuwa uingereza ni mojawapo wa nchi 123 zilizotia saini mkataba kuhusu mabomu yanayorushwa pamoja ambao hupiga marufuku utengenezaji au utumiaji wa mabomu hayo.

Waziri wa ulinzi wa uhispania Margarita Robles alisema kuwa nchi yake inadumisha msimamo kwamba aina fulani za silaha na mabomu hazifai kupelekwa nchini Ukraine.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *