Raila junior atawazwa kiongozi wa familia ya Raila Odinga

Martin Mwanje
1 Min Read
Mwanawe Raila Odinga, Raila Junior, akitawazwa kuwa kiongozi wa familia ya marehemu Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Mwanawe marehemu Raila Odinga, Raila Junior, leo Alhamisi ametawazwa kuwa kiongozi wa familia ya Waziri Mkuu huyo wa zamani. 

Utawazwaji huo unafuatia kifo cha kinara huyo wa zamani wa chama cha ODM wakati akipokea matibabu nchini India.

Kakake Raila, Oburu Oginga, anasema Raila Junior sasa yuko huru kushiriki mikutano ya familia pana ya marehemu Mzee Jaramogi Oginga Odinga kufuatia kutawazwa huko.

Mikutano hiyo huongozwa na Oburu Oginga, ambaye pia ni Seneta wa kaunti ya Siaya na kaimu kiongozi wa chama cha ODM.

Familia ya Raila bado inaomboleza kifo cha kiongozi huyo shupavu huku viongozi mbalimbali wakimiminika nyumbani kwake huko Bondo kuifariji familia.

Raila alizikwa Oktoba 19 baada ya kufariki akiwa na umri wa miaka 80.

Website |  + posts
Share This Article