Hatukubali shilingi bilioni 3 ng’oo! Wahadhiri waapa huku wakiendelea na mgomo

Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu umeingia wiki ya sita huku hali ya suitafahamu ikiendelea kughubika sekta ya elimu nchini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma kote nchini huenda wakasubiri kwa muda mrefu zaidi kabla ya kurejelea masomo.

Hii ni baada ya wahadhiri wa vyuo vikuu kukatalia mbali ofa ya shilingi bilioni 3.1, iliyotolewa na Tume ya Kuratibu Mishahara (SRC) ili kufutilia mbali mgomo wao.

Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, UASU, kimetaja pendekezo hilo la SRC kuwa kejeli na lisilo na mashiko kwenye majadiliano ya nyongeza mpya ya mshahara mwaka 2025-2029.

Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu umeingia wiki ya sita huku hali ya suitafahamu ikiendelea kughubika sekta ya elimu nchini.

Website |  + posts
Share This Article