Raia wa Uganda aandikisha rekodi ya kukumbatia mti kwa muda mrefu zaidi

Marion Bosire
1 Min Read

Faith Patricia Ariokot ndiye mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mtu aliyepiga mti pambaja kwa muda mrefu zaidi.

Ariokot ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi alishiriki zoezi hilo Januari 16, 2024.

Siku hiyo alivumilia na kuushikilia mti huo kwa muda wa saa 16 na dakika sita, likiwa jaribio la tatu la kuvunja rekodi yake ya kukumbatia mti kwa muda mrefu.

Alipokea habari kwamba kitambu cha rekodi za dunia cha Guinness kimekubalia na kusajili rekodi hiyo na sasa anasubiri cheti chake.

Ombi lake la rekodi yake kukubaliwa ni nambari 2305171328071 kulingana na ujumbe aliopokea kutoka kwa usimamizi wa “Guinness World Records”.

Binti huyo hangeweza kuficha furaha yake alipopata ujumbe huo na alitumia mtandao wa X kushukuru waliomuunga mkono.

Alisema haikuwa rahisi ikitizamiwa kwamba alijaribu mara tatu na hatimaye amefanikiwa.

Katika miaka ya hivi karibuni watu hasa wanaharakati wa mazingira wamekuwa wakikumbatia kitendo cha kukumbatia miti.

Kitendo hicho kinaaminika kuanzia nchini India mwaka 1973 katika eneo la Uttarakhand na kufahamika kama Chipko ambalo ni neno na kihindi linalomaanisha pambaja.

Share This Article