Vidosho wa Kenya waikomoa Uganda mechi ya kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya soka kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 17, Junior Starlets, imeanza vyema harakati za kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Uganda leo jioni.

Mchuano hjuo wa raundiu ya pili mkumbo wa kwanza ulisakatwa katika uchanjaa wa Nakivubo jijini Kampala Uganda.

Edinah Nasipwondi na Joan Ogolla walipachika baoa moja kila mmoja kuanko dakika za 36 na 46 na kuipa Kenya ushindi maridhawa.

Vidosho wa Kenya chini ya ukufunzi wa Mildred Cheche, watawaalika Uganda kwa mkumbo wa pili wikendi ijayo huku mshindi wa jumla akifuzu kwa raundi ya tatu.

Kenya inapania kufuzu kwa fainali hizo kwa mara ya pili mtawalia, baaada ya kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka jana katika Jamhuri ya Dominica.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *