Timu ya Kenya ya raga kwa wanawake saba kila upande imeichachafya Colombia alama 12-5, katika nusu fainali ya mkondo wa pili wa mashindano ya HSBC Sevens Challenger mjini Cape Town, Afrika Kusini.
Ushindi huo umedumisha matokeo bora ya Kenya kutopoteza mechi tangu mkondo wa kwanza wiki jana.
Kenya maarufu kama Lionesses,sasa itamenyana na wenyeji Afrika Kusini kwenye fainali ya baadaye Jumamosi usiku.
Wenyeji walifuzu kwa fainali kufuatia ushindi wa pointi 21-15 dhidi ya Jamhuri ya Czech, katika nusu fainali.
Kenya ilitwaa ubingwa wa mkondo wa kwanza wa mashindano hayo wiki iliyopita.