Raia wa Taiwan wapiga kura kumchagua Rais na wabunge

Tom Mathinji
1 Min Read

Takribani raia milioni 19.5 wa Taiwan wanapiga kura kumchagua rais mpya na wabunge leo Jumamosi, kwenye uchaguzi muhimu kwa mustakabali wa kisiwa hicho kuhusu uhusiano wake na Uchina.

Taiwan ni eneo huru la kidemokrasia linalojitawala japo Uchina imekuwa ikidai kisiwa hicho ni eneo lake ambalo pia halijatambuliwa na jamii ya kimataifa kama taifa huru.

Chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP) kinachotafuta utawala kwa muhula wa tatu, kimekuwa kikikabiliana na serikali ya Uchina kuhusu uhuru wa Taiwan.

Mwaniaji wake William Lai ametajwa kama mkorofi na Uchina ambayo ilitoa wito kwa raia wa eneo hilo kutompigia kura.

Kwa upande mwingine chama cha upinzani Kuomintang au KMT, kimeahidi kuleta uhusiano mwema na Uchina na kuboresha Amani katika kisiwa cha Taiwan.

TAGGED:
Share This Article