Mfalme Willem-Alexander na Malkia Máxima wa Uholanzi wawasili Kenya kwa ziara rasmi

Dismas Otuke
1 Min Read

Mfalme Willem Alexander na Malkia Maxima, wamewasili nchini Kenya Jumatatu usiku kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku nne.

Mfalme na Malkia walilakiwa na Naibu Rais Kithure Kindiki, na Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe, punde walipotua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Ndge iliyowabeba ilitua uwanja wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili usiku, baada ya kuitikia mwito wa Rais William Ruto wa kuzuru Kenya.

Wakiwa nchini wanatarajiwa kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano katika sekta ya utalii, biashara, kilimo na usafari pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Rais Ruto na Mkewe Bi Rachal wanatarajiwa kuwakaribisha viongozi hao wawli wa Kifalme katika Ikulu kesho kwa sherehe rasmi mapema asubuhi na kusaini mikataa kadhaa, kabla ya kushiriki upanzi wa miti ,kuzungumza na vijana katika msimu wa Thogoto na hatimaye kushiriki dhifa ya chajio.

Website |  + posts
Share This Article