Raia sita wa Iran walifikishwa mahakamani Shanzu Oktoba 27, kujibu mashataka ya kulangua dawa za kulevya za thamani ya shilingi bilioni 8 za Kenya.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma amewashtaki Jasem Darzadeh Nia, Nadeem Jadgal, Imran Baloch, Hassan Baloch, Rahim Baksh na Imtiyaz Daryayi baada ya kukamatwa na Jeshi wa Wanamaji tarehe 24 mwezi huu katika Bandari ya Kilindini wakiwa na makasha 769 ya kilo 1,035.9 za mihadarati.
Kiongozi wa mashtaka ya umma anatarajiwa kuiomba mahakama kuwazuia washukiwa kwa siku 30 zaidi, kuruhusu kukamilishwa kwa uchunguzi wakati kesi itakapokatajwa Jumanne, Oktoba 28.