Queen Ifrica amzomea waziri Olivia Grange

Mwanamuziki huyo anahisi kwamba mambo anayosimamia waziri huyo ya Jinsia, Burudani, Utamaduni na Michezo hayaendeshwi vyema.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Jamaica, Queen Ifrica, ametuma ujumbe wa dhati kwa Waziri wa Jinsia, Burudani, Utamaduni na Michezo nchini humo Olivia Grange, akilalamikia kudorora kwa nguzo za utamaduni na kijamii za Jamaica.

Katika barua ya wazi kupitia mitandao ya kijamii, Ifrica alikosoa vikali kusambaratika kwa usawa wa kijinsia, burudani, michezo na maadili ya kitamaduni chini ya uongozi wa Grange.

Alilalamika kwamba hadhi ya wanawake inapuuzwa na wanamichezo wa Jamaica kama Usain Bolt wanakosa kutambuliwa. Alieleza pia kukerwa kwake na kuharibiwa kwa urithi wa kitamaduni wa Jamaica akitaja hali hiyo kuwa “aibu kubwa”.

“Je, hili sio jambo la kujiuliza?” alishangaa Ifrica akiuliza iwapo mabadiliko haya ni sehemu ya mpango wa kimakusudi.

Alimkumbusha Grange kuhusu nafasi ya Jamaica katika harakati za kimataifa, akimhimiza akumbuke historia ya taifa hilo ya kupigania uhuru, ikiwa ni pamoja na kupinga ubaguzi wa rangi.

Kwa hisia kali Ifrica alionya kwamba mwelekeo huu wa sasa unaweza kuhatarisha urithi wa kisiwa hicho na mababu zao. “Mungu hapendezwi,” alimaliza, akimhimiza waziri kuwazia upya namna anavyofanya kazi yake kabla muda haujakwisha.

Ujumbe wa mwanamuziki huyo wa kike wa Jamaica umezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, na wengi wakiunga mkono wito wake wa kurejelea mizizi ya Jamaica.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *