Putin: Tuko tayari kutumia silaha za nyuklia

Marion Bosire
1 Min Read

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kwamba nchi yake iko tayari kabisa kutumia sialaha za Nyuklia iwapo uhuru wa nchi hiyo utatishiwa kwa vyovyote.

Aliyasema haya kwenye mahojiano yaliyopeperushwa leo kwenye runinga ya kitaifa ya Rossiya-1, katika kile kinachoonekana kuwa hatua ya kurejelea vitosho vya kutumia wanajeshi na sialaha kali.

Haya yanajiri wakati raia wa nchi hiyo wanajiandaa kwa uchaguzi wa Urais wikendi hii.

Wiki mbili zilizopita kiongozi huyo alisema kwamba kulikuwa na tishio la vita vya nyuklia iwapo nchi za magharibi zingeamua kutuma wanajeshi wao kupigana nchini Ukraine.

Leo amesisitiza kwamba uwezo wa urusi katika silaha za nyuklia na wanajeshi ni bora kuliko wa nchi za magharibi.

Putin pamoja na viongozi wengine wa Urusi wana hulka ya kusifia uwezo wa nchi hiyo katika zana za nyuklia tangu nchi hiyo ilipovamia Ukraine Februari 2022.

Hata hivyo viongozi hao husema kwamba ukumbusho huo haufai kuchukuliwa kuwa vitisho.

Putin aligusia uwezo finyu wa kitaalamu wa Marekani katika masuala ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na katika kujizuia kimkakati.

Website |  + posts
Share This Article