Profesa Kiama arejeshwa likizo na bodi ya Chuo Kikuu cha Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi Profesa Stephen Kiama ametumwa kwa likizo ya lazima na bodi ya chuo hicho, mwezi mmoja baada ya kurejea afisini kutoka kwa likizo ya lazima ya miezi sita.

Kulingana na taarifa kutoka kwa chuo hicho, Prof. Kiama ameonywa kutotekeleza majukumu yoyote chuoni humo kuanzia Septemba 25 mwaka huu.

Kumekuwa na utata wa uongozi chuoni humo tangu Prof. Kiama arejee kutoka likizo aliyoanza Agosti mosi.

Alitarajiwa kurejea kazini baada ya likizo hiyo ili  kukamilisha mkataba wake.

Hata hivyo, Profesa Kiama alirejea kazini baada ya siku 30 pekee.

Share This Article