Polisi waimarisha vita dhidi ya magenge ya wahalifu Nairobi

Kufuatia habari za kijasusi, maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kayole Jijini Nairobi, wamewakamata washukiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na wizi wa simu na uuzaji wa simu zilizoibwa.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi waimarisha vita dhidi ya wizi wa simu za mkononi.

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS imeimarisha vita dhidi ya magenge yanayohusika na wizi wa simu za mkononi na biashara haramu ya simu zilizoibwa.

Kufuatia habari za kijasusi, maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kayole jijini Nairobi, wamewakamata washukiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na wizi wa simu na uuzaji wa simu zilizoibwa.

Wanne hao walikamatwa kwenye operesheni iliyotekelezwa na maafisa polisi katika eneo la Nyaura mtaani Kayole.

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na mshukiwa anayedaiwa kupokea simu zilizoibwa, watatu wakiwa washukiwa wa wezi wa simu.

Kwenye ukurasa wa X, NPS ilisema operesheni hiyo ilisababisha kupatikana kwa simu 132, vifaa vya simu na tarakilishi mbili zinazoaminika kufanikisha uhalifu huo.

“Operesheni hiyo inaashiria kujitolea kwa NPS kusambaratisha magenge ya wahalifu na kuwalinda wananchi dhidi ya uhalifu,” ilisema huduma hiyo.

Share This Article