Polisi wameanza kuwatafuta maafisa wawili wa halmashauri ya ushuru nchini, KRA wanaohofiwa kufariki kwenye mafuriko katika kaunti ya Kwale Ijumaa usiku baada ya gari lao kusombwa na maji karibu na mto Ramisi.
Mafuriko makubwa yameshuhudiwa katka ukanda wa pwani juma hili kutokana na viwango vikubwa vya mvua vinavyoshuhudiwa.
Hali hiyo imesababisha watu wengi kupoteza makazi huku serikali kuu ikitangiwa kuingilia kati upesi kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.