Waandalizi wa michuano ya kombe la Euro mwaka ujao Ujermani waliendeleza msururu wa matokeo duni walipoambulia kichapo cha goli moja kwa nunge dhidi ya Poland, katika mechi ya kimataifa ya kirafiki ilyochezwa Ijumaa usiku.
Jakub Kiwior alipachika goli pekee kwa wenyeji Poland ,kipigo kinachoongeza masaibu ya Wajerumani ambao wameshinda mechi tatu pekee kati ya 10 za hivi punde.
Ujerumani watachuana na Colombia wiki ijayo huku wakiwa na chini ya mwaka mmoja kujiandaa kwa fainali za kombe la Euro.