Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC imeendelea kuadhimisha juma la kusherehekea mafanikio yaliyoafikiwa tangu umoja huo kuanza. Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, maeneo kame na maendeleo ya kikanda nchini Penina Malonza katika mahojiano na Pepea Mashariki amesema uhusiano mwema kati ya mataifa na ukuzaji biashara ni miongoni mwa mambo ambayo jumuiya hiyo inajivunia.
https://art19.com/shows/taarifa/episodes/e55441a5-d1a8-48b4-958b-9389b170ac02