Paul Kagame awasilisha stakabadhi zake kuwania Urais kwa mara ya nne

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Paul Kagame awasilisha stakabadhi zake kuwania Urais mwezi July.

Rais Paul Kagame alikuwa wa kwanza kuwasilisha nyaraka zinazohitajika ili kumuwezesha kuwa mgombea wa nafasi ya sasa ya rais wa Rwanda.

Akiwa na mkewe Jeannette Kagame na katibu wa chama cha FPR-Inkotanyi na maafisa wengine, Paul Kagame alipokelewa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Oda Gasinzigwa ambaye alimkabidhi stakabadhi zinazohitajika na tume hiyo.

Kipindi cha kupokea wagombea wa urais wa Jamhuri au wabunge kilianza siku ya Ijumaa na kitadumu kwa karibu wiki mbili.

Wagombea wengine wanaotarajiwa kuwasilisha nia zao katika muda wa wiki mbili zijazo ni pamoja na Frank Habineza wa Chama cha Rwanda cha Demokrasia na Ulinzi wa Mazingira, na mgombea binafsi Diane Rwigara, kutoka chama cha upinzani.

Share This Article