Inspekta Jenerali atoa taarifa kuhusu ajali ya barabara ya Ngong

Ajali hiyo inaripotiwa kutokea wakati msafara wa Rais ulikuwa ukielekea katika mtaa wa Kibera.

Marion Bosire
1 Min Read

Afisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja imetoa taarifa kuhusu ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Adams Arcade kwenye barabara ya Ngong jijini Nairobi.

Ajali hiyo ilihusisha gari la serikali na ilisababisha kifo cha mtu mmoja ambaye amebainika kuwa raia wa kigeni.

Katika taarifa iliyotiwa saini na Muchiri Nyaga ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano na msemaji wa huduma ya taifa ya polisi, suala hilo sasa linashughulikiwa na huduma ya taifa ya polisi.

Nyaga amehimiza umma kutoa taarifa ambazo zinaweza kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo ambao anasema umeanzishwa. Walio na taarifa wanaweza kuziwasilisha katika vituo vya polisi vilivyo karibu.

Wanaweza pia kupiga simu kwa nambari ambazo hazitozwi malipo yoyote za 999, 911 na 112.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *