Kimanzi ateuliwa Mkurugenzi wa kiufundi FKF

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa kaimu kocha wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Francis Kimanzi, ameteuliwa kuwa mkurugenzi mpya wa kiufundi wa shirikisho la soka nchini FKF.

Akitangaza uteuzi huo, Katibu Mkuu wa Shirikihso Harold Ndege alisema ana imani na utendakazi wa Kimanzi, kutokana na tajiriba pana aliyo nayo katika masuala ya usimamizi wa kandanda nchini.

Kimanzi amekuwa kaimu kocha wa Harambee Stars tangu mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya kuachia uongozi wakati Benni McCarthy alipoteuliwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *