Ratiba ya robo fainali kuwania Ligi Mabingwa Ulaya yakamilika

Dismas Otuke
1 Min Read

Ratiba ya mechi za robo fainali kuwania taji ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, imebainika kufuatia kukamilika kwa michuano ya raundi ya 16 bora jana usiku.

Arsenal wanapowania taji ya kwanza, watawaalika mabingwa watetezi Real Madrid, katika duru ya kwanza ya kwota fainali tarehe 8 mwezi ujao.

Bayern Munich wataanzia nyumbani dhidi ya Intermilan ya Italia pia April 8.

Barcelona watawatumbuiza Borusia Dortmund kutoka Ujermani ,kwenye mkumbo wa kwanza tarehe 9 mwezi ujao wakati Paris St Germain ya Ufaransa, ikipimana nguvu na wageni Aston Villa, katika duru ya kwanza tarehe 9 April.

Michuano ya marudio ya kwota fainali itasakatwa tarehe 15 na 16 mwezi ujao huku timu zitakazoibuka na ushindi zikifuzu kwa nusu fainali.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *