Limbukeni Cape Verde watachuana na mabingwa watetezi Argentina, Ijumaa ijayo Julai 3,kwenye raundi ya 32 ya fainali za Kombe la Dunia.
Pambano hilo litakuwa sawia na hadithi ya Bibilia ya Daudi na Goliath, kwani Argentina wanaoongozwa na Lionel Messi ni timu bora duniani wakiwa wamenyakua kombe hilo mara mbili.
Upande wao Blue Sharks kutoka visiwani Cape Verde, wanashiriki kwa mara ya kwanza na waliweka historia kwa kutoka sare tasa na Uhispania,kwenda sare ya 2-2 na Uruguay, na kutoka sare kappa na Saudi Arabia kundini H.
Endapo wataandikisha historia zaidi kwa kuibandua Argentina, au watayaaga mashindano,tayari Cape Verde wamejituma kibabe na kuweka juu bendera ya Afrika katika Kombe la Dunia.