Owalo awatuza Gor Mahia shilingi milioni 3

Dismas Otuke
1 Min Read

Gor Mahia wana kila sababu ya kutabasamu baada ya waziri Teknolojia ya Habari na mawasiliano na uchumi wa Kidijitali Eliud Owalo, kuwatuza shilingi milioni 3, baada ya kunyaku ubingwa wa ligi kuu ya Kenya kwa mara ya 20 siku ya Jumapili.

Owalo aliwandalia wachezaji na maafisa wa benchi ya kiufundi chakula cha mchana kuwapongeza kufuatia ushindi wa kihistoria walipoicharaza Nairobi City Stars mabao manne kwa moja katika mechi ya kufunga msimu na kunyakua taji ya ligi kuu .

Gor Mahia walitawazwa mabingwa aada ya kuzoa pointi 70 kutokana na mechi 34 ,alama moja zaidi ya Tusker FC waliomaliza katika nafasi ya pili.

Waziri Owalo ambaye ni mlezi wa Gor Mahia amekuwa akiisaidia klabu hiyo kwa hali na mali msimu uliomalizika.

Ushindi wa ligi kuu unawapa tiketi ya kushiriki kinyang’anyiro cha ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao.

Takrima ya Owalo ni afieni kubwa baada ya shirikisho la soka nchini FKF kutangaza kuwa hakutakuwa na tuzo ya pesa kwa mabingwa wa ligi kuu msimu uliomalizika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *